Zaidi ya tafiti 149 kuhusu bibi Zainabu (a.s) zimewasilishwa kwenye kongamano la Ruhu-Nubuwah na kuingizwa katika maktaba ya elimu

Kongamano la Ruhu-Nubuwah awamu ya tano limekuwa na mada zaidi ya 149 zinazohusu bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kutoka ndani na nje ya Iraq zimeingizwa katika maktaba ya elimu.

Kongamano hilo husimamiwa na idara ya shule za Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, mada zake zimejikita katika maeneo nane, miongoni mwa maeneo hayo ni historia ya bibi Zaharaa (a.s) na athari yake katika elimu.

Kwa mujibu wa wasimamizi wa kongamano hilo, hakika ni fursa ya kushajihisha watafiti kuangazia utukufu wa bibi Zaharaa (a.s) sambamba na mafunzo ya uislamu kwa ujumla katika kujenga familia bora.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: