Kongamano la Ruhu-Nubuwah la kitamaduni na kimataifa awamu ya tano limeshuhudia shughuli za kielimu na kitamaduni, na limepata muitikio mkubwa ndani na nje ya Iraq.
Kongamano hilo limeandaliwa na idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya na limehusisha maonyesho ya picha, mabango ya kuchorwa na hati za kiarabu.
Pembeni ya kongamano hilo yamefanywa maonyesho ya vitu mbalimbali, usomaji wa Qur’ani, nadwa, maigizo na vikao vya usomaji wa mashairi, mambo yato yalikua yanaangazia historia ya bibi Zaharaa (a.s).
Kongamano limedumu kwa muda wa siku nne, likiwa ni sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya mazazi ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s), na kubainisha namna Atabatu Abbasiyya inavyo thamini jambo hilo sambamba na kuwasilisha ujumbe wa Mtume Muhammad s.a.w.w) kwa walimwengu wote.