Katika kongamano la Ruhu-Nubuwah.. vitu vingi vimeshuhudiwa katika maonyesho ya kazi za mikono

Maonyesho ya kazi za mikono yanayofanywa pembeni ya kongamano la Ruhu-Nubuwah awamu ya tano yameshuhudia vitu tofauti (300).

Kongamano linakauli mbiu isemayo (Bibi Zaharaa -a.s- ni turathi takatifu ya kujivunia) limesimamiwa na idara ya shule za Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Maonyesho yamedumu kwa muda wa siku mbili, yalikua na vitu tofauti, miongoni mwa vitu hivyo ni: vifaa vya urembo, vibakuli vya mishumaa, vitambaa vilivyo dariziwa, uchoraji wa vikombe na mabango ya picha, ni fursa nzuri ya kuonyesha ubunifu wa wanawake, sambamba na kuwepo kwa mazingira ua ushindani baina ya washiriki.

Yamefanywa mashindano katika vitu vitatu (Pisha bora ya mnato, kazi nzuri ya kiufundi na bango lenye picha nzuri).

Waliofanya vizuri katika maonyesho hayo ni Amirah Abdu-Ali katika vifaa vya urembo, Furqani Abdurazaaq katika uchoraji wa vikombe, As’ad Ali katika mishumaa, Zaharaa Hussein Majidi katika fani ya kudarizi na Ghadiir Nasoro Hussein katika mapambo ya vibakuli vya mishumaa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: