Jumuiya ya Al-Ameed imehitimisha warsha kuhusu ombaomba

Jumuiya ya Al-Ameed kwa kushirikiana na baraza la mawakili wamefanya mazungumzo na vyombo vya serikali chini ya ulezi wa Atabatu Abbasiyya kuhusu kuongezeka kwa ombaomba mitaani.

Warsha hiyo imepewa jina la (kuweka mkakati wa kitaifa wa kupambana na muinekano mbaya unaoanza kujitokeza katika jamii), wameshiriki watafiti wengi.

Katika warsha hiyo imeonyeshwa filamu ya kielelezo cha kuwepo kwa ombaomba mitaani, kisha Dokta Ali Abdul-Azizi Alyaasiri mkuu wa kituo cha kitaifa cha mikakati ya amani ya umma akatoa mada isemayo (mbinu za kupambana na ombaomba hapa Iraq).

Katika warsha hiyo yamejadiliwa mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni Uchumi, Sheria, Utamaduni, Jamii pamoja na mambo mengine.

Warsha ikahitimishwa kwa kuweka maazimio yanayotakiwa kufanyiwa kazi na kuondoa tatizo la ombaomba hapa nchini, sambamba na kugawa vyeti vya ushiriki kwa baadhi ya viongozi walioshiriki kwenye warsha hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: