Kitengo cha habari na utamaduni na wakfu Shia wamejadili njia za kuthibitisha jinai za magaidi

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kupitia kituo cha kiiraq cha kuthibitisha jinai pamoja na wakfu Shia, wamejadili njia za kuthibitisha jinai za magaidi.

Yamesemwa hayo wakati makamo kiongozi mkuu wa wakfu Shia Sayyid Hussein Jihadi Hassaani alipotembelea ofisi za kituo cha kuthibitisha jinai za magaidi mjini Najafu.

Mkuu wa kituo hicho Dokta Abbasi Quraishi amesema “Kikao chetu kimejadili mambo mengi yanayohusu jinai za magaidi zinazotokea hapa Iraq na kugharimu maisha ya watu wengi”.

Makamo kiongozi mkuu wa wakfu Shia amepongeza kazi kubwa inayofanywa na kituo cha kuthibitisha jinai za magaidi, kwani ndio kituo cha kwanza kufanya kazi hiyo ya kusajili jinai walizofanyiwa wananchi wa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: