Sayyid Swafi ampa zawadi mshindi wa kwanza wa shindano la Qur’ani la kitaifa

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amempa zawadi mshindi wa kwanza wa shindano la Qur’ani la kitaifa awamu ya nane kwa vyuo vikuu vya Iraq, msomaji Ali Zubaidi.

Msomaji wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ali Zubaidi amekuwa mshindi wa kwanza kwenye shindano la kuhifadhi Qur’ani lilikua na washiriki zaidi ya (33).

Sayyid Swafi amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Majmaa-Ilmi, akahimiza waendelee kuibua vipaji vya usomaji wa Qur’ani.

Zawadi hiyo imetolewa mbele ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Murtadha Aali Dhiyaau-Dini, mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Afdhalu Shaami, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, rais wa Majmaa-Ilimi Dokta Mustaaqu Ali na mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu Sayyid Muhandi Almayali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: