Sayyid Swafi azawadia watumishi wa kitengo cha Habari baada ya kutoka semina nchini Tunisia

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amewapa zawadi watumishi wa kituo cha Alfadhil kinacho husika na kutunza nakala-kale na vielelezo vya kihistoria chini ya kitengo cha habari na utamaduni, baada ya ushiriki wao kwenye semina iliyofanyika nchini Tunisia.

Semina hiyo imefanywa katika mji wa Qirawani nchini Tunisia, ilikuwa na washiriki kutoka nchi nane ikiwemo na Iraq, amesema hayo muwakilishi wa kituo cha Alfadhil cha kutunza nakala-kale na vielelezo vya kihistoria katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Sayyid Swafi amesisitiza umuhimu wa kushiriki kwenye matukio ya kimataifa, kupitia kitengo cha habari na utamaduni au vitengo vingine, kutokana na ukweli kuwa ni fursa ya kujipima na kuona tulipofika.

Mheshimiwa akapongeza ubunifu wa raia wa Iraq wanapopewa nafasi stahiki, akabainisha kuwa Atabatu Abbasiyya inafanya kazi wakati wote ya kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi kwa vitengo vyote, ili viweze kutangaza utamaduni wa Ahlulbait (a.s).

Zawadi zimetolewa mbele ya katibu mkuu Sayyid Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, makamo katibu mkuu, mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Afdhalu Shami, wajumbe wa kamati kuu na msimamizi wa semina iliyofanywa nchini Tunisia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: