Kikundi cha wasichana.. kituo cha utamaduni wa familia kinatoa mhadhara wa namna ya (kutumia muda)

Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya, kinatoa mhadhara kuhusu namna ya (kutumia muda) kwa kundi la wasichana wa mkoa wa Karbala.

Mtoaji wa mhadhara alikua ni bibi Salma Hamdi, ameongea kuhusu umuhimu wa kupanga muda katika utendaji wa majukumu ya nyumbani, ili kupata furaha na utulivu katika familia.

Kituo cha utamaduni wa familia kimekua kikitoa mihadhara hii kwa wasichana wa mkoa wa Karbala wenye umri tofauti mara mbili kwa mwezi, lengo la mihadhara hii ni kuwataka wafuate mwenendo mtukufu wa bibi Zainabu (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: