Kitengo cha Dini kimesema: Tumefungisha zaidi ya ndoa elfu 6 katika mwaka wa 2022m

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimesema kuwa mwaka (2022m) kimefungisha zaidi ya ndoa (6000).

Idara ya mikataba na ndoa chini ya kitengo cha Dini, imefungisha ndoa (6197) ndani na nje ya mkoa wa Karbala ndani ya miezi kumi tu, ukitoa mwezi wa Muharam na Safar.

Idara inajukumu la kufingisha ndoa ndani ya eneo la haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kutoa maelezo kwa wanandoa na familia zao, kisha husomwa hutuba ya ndoa kwa sauti inayosikika kwa lugha ya kiarabu fasaha, hayo hufanywa na aliyepewa jukumu la kufungisha ndoa.

Kisha wanandoa hupewa cheti cha ndoa huku nakala nyingine ikitunzwa na idara ya ufungishaji wa ndoa, kumbuka ndoa inayofungwa Atabatu Abbasiyya inatambuliwa na serikali ya Iraq kwa mujibu wa sheria za Iraq.

Tambua ndoa inayofungwa Atabatu Abbasiyya ina athari kubwa sana katika nafsi za waumini, kutokana na utukufu wa eneo hilo takatifu, hakika waumini huja katika eneo hili wakati wa furaha zao kabla ya huzuni, nao ni utamaduni uliozoweleka kwa familia nyingi za Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: