Kwenye uwanja wenye ukubwa wa mita 2250.. chuo kikuu cha Alkafeel kinajenga kitivo cha udaktari wa binaadamu

Chuo kikuu cha Alkafeel katika mji wa Najafu kinajenga kitivo cha udaktari, baada ya kupewa kibali na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.

Chuo kimeruhusiwa kujenga kitivo hicho baada ya kukamilisha vigezo vyote, kitivo hicho ni sehemu ya maendeleo ya kielimu hapo chuoni.

Kitivo kimeanzishwa chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, aliyesisitiza umuhimu wa kukamilisha mahitaji muhimu yote katika uboreshaji wa elimu.

Kitivo hicho kitakuwa na hospitali maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vitendo, sambamba na kuajiri walimu bora na bobezi kwenye fani zao.

Eneo linaukubwa wa mita za mraba elfu mbili mia mbili na hamsini, jengo linaghorofa sita zenye ukubwa wa mita elfu kumi na tatu na miatano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: