Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua jukumu la kukarabati nyumba ya familia ya watu wa Karbala baada ya kubomoka katika kitongoji cha Huru ndani ya mkoa wa Karbala.
Muwakilishi wa ugeni kutoka Ataba tukufu Sayyid Adnani Jalukhani Mussawi amesema “Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi ameagiza kukarabati nyumba iliyobomoka ya familia hiyo, alitoa agizo hilo baada ya ujumbe wa Ataba kutembelea majeruhi waliotokana na ajali hiyo waliolazwa kwenye hospitali ya mji wa Imamu Hussein katika mji wa Karbala”.
Akaongeza kuwa “Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya umeenda kuwajulia hali wahanga na kuangalia namna ya kuwasaidia, akabainisha kuwa wahanga wa tukio hilo ni mtoto wa kiume na mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 9, wote wanaendelea vizuri kwa sasa”.