Nchini Kamerun.. Kitengo cha Habari na utamaduni kinafanya hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Zaharaa (a.s)

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimefanya hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) mashariki ya mji mkuu wa Kamerun.

Hafla hiyo imesimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo tajwa.

Mkuu wa Markazi Shekhe Saad Sataar Shimri amesema: “Katika hafla hiyo yametolewa mawaidha kuhusu utukufu wa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) katika uislamu, wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wamehudhuria kwa wingi”.

Akaongeza kuwa “Hafla ilikua na vipengele vingi ikiwa ni pamoja na ugawaji wa zawadi na chakula kwa wahudhuriaji”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: