Ujumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano la bibi Zaharaa umekutana na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Husseiniyya tukufu

Ujumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa awamu ya pili la Fatuma Zaharaa (a.s) umekutana na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya Mheshimiwa Shekhe Abdulmahadi Karbalai.

Ujumbe huo umeongozwa na Sayyid Rasuulu Mussawi ambaye ni muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mkoa wa Baabil na msimamizi mkuu wa kongamano, litakalofanywa katika Maqaam ya muujiza wa kurejeshwa jua (Radu-Shamsi) kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kituo cha turathi za Hilla na chuo kikuu cha Baabil.

Sayyid Mussawi akaeleza kwa muhtasasi kuhusu maandalizi ya kongamano na mchango wa kila kamati, pamoja na kueleza idadi ya mada zitakazo wasilishwa sambamba na kueleza picha ya baadae ya kongamano la awamu ya tatu na maazimio muhimu yatakayo yanyiwa kazi.

Naye Mheshimiwa Shekhe Karbalai akatoa baadhi ya mapendekezo na mtazamo wake katika kongamano la awamu ya tatu, akashauri kupanua wigo wa kushirikisha vyuo vikuu na Maahadi zilizopo kwenye mkoa huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: