Waziri wa elimu ya juu na tafiti za kielimu amesema: Chuo kikuu cha Alkafeel ni miongoni mwa miradi muhimu ya kimkakati

Waziri wa elimu ya juu na tafiti za kielimu Dokta Naim Al-Abudi amesema kuwa Chuo kikuu cha Alkafeel ni mradi muhimu wa kimkakati.

Wakati wa uzinduzi wa kitivo cha udaktari wa binaadamu amesema kuwa “Hakika chuo kikuu cha Alkafeel ni mradi muhimu wa kimkakati, wizara imesha kipasisha chuo hiki na leo tumeona kikiwa katika ubora mkubwa kimajengo, kielimu, kinidham, kiratiba na walimu wake ni wazuri zaidi”.

Akaongeza kuwa “Ni wazi kuwa maamuzi yetu ya kufungua chuo hiki hayakuwa mabaya, yalikuwa mazuri yenye faida kubwa kwa wizara”.

Akasisitiza kuwa “Miradi ya Ataba tukufu, sawa iwe Atabatu Husseiniyya au Abbasiyya, ni miradi muhimu kwa jamii”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Al-Abudi, hakika wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu inaunga mkono hatua zote za maendeleo na zenye matokeo chanya zinazoweza kuigwa na vyuo vikuu vingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: