Idaya ya wahadhiri wa Tablighi katika Atabatu Abbasiyya, imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Alhadi (a.s) mbele ya kundi kubwa la mazuwaru.
Mihadhara mbalimbali inatolewa kwenye majlisi hiyo, na itaendelea kufanywa kwa muda wa siku tatu.
Mhadhiri wa majlisi Sayyid Mansuur Qashaqish amesema “Mada imejikita katika kueleza nafasi ya Imamu Alhadi (a.s) katika kulinda uislamu, na historia yake tukufu, namna alivyo hama Madina na Kwenda Samaraa, alikoishi akiwa ametengwa na familia yake pamoja na wafuasi wake”.
Atabatu Abbasiyya imepandisha bendera za uombolezaji zilizo andikwa maneno yanayo ashiria msiba ndani ya haram tukufu, kama sehemu ya kumpa pole Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).