Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya kwa kushirikiana na kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s), imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali Alhadi (a.s).
Majlisi hiyo imefanywa asubuhi ya Alkhamisi (26/01/2023m), na kufunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha ikasomwa ziara ya maasumina (a.s).
Yakafuata mawaidha yaliyotolewa na mhadhiri bibi Zainabu Abdulhadi yaliyokua na anuani isemayo: (Imamu Alhadi “a.s” jambo lake ni la Mwenyezi Mungu), ameongea mambo mengi, miongoni mwa aliyo ongea ni utukufu wa Imamu Alhadi (a.s), historia yake na mpangilio wa maimamu (a.s).
Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma kaswida za kuomboleza na Duaa-Faraj ya Imamu wa zama (a.f).