Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendelea kutoa semina za (Answarul-Kafeel) kwa watumishi wa Ataba tukufu.
Mkufunzi Shekhe Abdulsataar Alhajami amesema “Lengo la semina zinazo andaliwa chini ya ratiba ya Answarul-Kafeel, ni kuwajengea uwezo watumishi katika masomo ya Fiqhi, Aqida na Akhlaq”.
Akaongeza kuwa “Semina ya wiki hii imewalenga watumishi wa idara ya vyoo kutoka kitengo cha utumishi, itadumu kwa muda wa siku tano, wanafundishwa masomo ya Fiqhi yanayohusu watumishi na mwisho wa semina watapewa mtihani”.
Ratiba ya Answarul-Kafeel inalenga kuwajengea uwezo watumishi wa Atabatu Abbasiyya katika elimu ya Dini utamaduni na Akhlaq.