Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake inafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Alhadi (a.s)

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, inafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Alhadi (a.s).

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema: “Kutokana na kauli ya Maasum isemayo (Huisheni mambo yetu, Mwenyezi Mungu amrehemu atakayehuisha mambo yetu), tumefanya majlisi ya kuomboleza msiba huu”.

Akaongeza kuwa “Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu na ziara ya Imamu Alhadi (a.s) iliyofuatiwa na mawaidha yaliyojikita katika kueleza mambo muhimu yaliyotokea wakati wa uhai wake (a.s)”.

Majlisi ikahitimishwa kwa kusomwa kaswida na tenzi za kuomboleza pamoja na duaa-Faraj ya kuomba kudhihiri haraka kwa Imamu Mahadi (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: