Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kupitia kituo cha turathi za Hilla, kimepokea ugeni kutoka Atabatu Husseiniyya tukufu.
Wamejadili harakati zinazofanywa na kituo, na mafanikio muhimu yaliyopatikana miaka ya nyuma, sambamba na mbinu za kutekeleza malengo ya kituo katika sekta ya utunzi na uandishi.
Ugeni umepongeza kazi nzuri inayofanywa na kituo katika sekta ya elimu, ukawataka waendelee na kazi hiyo tukufu ya kuhuisha turathi za wanachuoni wa madrasa ya Ahlulbait (a.s).