Kwa mubalighina waafrika.. kitengo cha Habari na utamaduni kinafanya semina ya kujenga uwezo

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya semina ya mubalighina wa kiafrika kwa ajili ya kuandaa miradi ya kitamaduni na kimkakati.

Semina hiyo imelenga wanafunzi wa Dini kutoka nchi za Afrika na kusimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya.

Mkuu wa Markazi (kituo) Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema “Markazi hufanya kila iwezalo katika kujenga uwezo wa kielimu kwa wanafunzi wanaotoka nchi za Afrika, kwa kufanya semina mbalimbali. Mhadhiri wa semina hiyo alikua ni Dokta Muhammad Jaasim, ameongea kuhusu mikakati ya kuandaa miradi ya kitamaduni”.

Akafafanua kuwa “Semina inalenga kueleza mikakati na mpango kazi wa miradi ya kitamaduni na kielimu, na matokeo chanya katika kufanikisha miradi na malenngo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: