Mpiga picha wa Atabatu Abbasiyya tukufu bwana Azharu Hamidi Asadi, amepata tuzo ya ubora na tuzo ya shindano lililoendeshwa na jumuiya ya wapiga picha wa Iraq.
Rais wa jumuiya ya wapiga picha wa Iraq Sayyid Haadi Najaari amesema “Shindano linaumuhimu mkubwa, washiriki wanatoka miji tofauti ya Iraq na wenye umri tofauti, jumla ya washiriki walikuwa (1500), picha (220) zimefanya vizuri na kukubaliwa”.
Akaongeza kuwa “Jumla ya zawadi (44) zimetolewa katika makundi matatu, ambayo ni: kundi la rangi, ubainifu wa rangi na kundi la magazeti, ushiriki wa wapiga picha ulikuwa mkubwa”.
Naye mpiga picha bwana Azharu amesema “Nimefaulu kupitia kundi la magazeti na ubainifu wa rangi, na nimepewa tuzo la ubora kutoka muungano wa wapiga picha wa kimataifa”.
Kwa mujibu wa Asadi, hakika ushindi huo unatokana na msaada endelevu wa Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya na idara ya Habari, wao ndio chachu ya kuwa na mafanikio katika sekta ya picha hapa Ataba.