Chuo kikuu cha Alkafeel kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali Alhadi (a.s)

Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali Alhadi (a.s).

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Dhulfiqaar Saaburi kisha akapanda kwenye mimbari shekhe Abdullahi Dujaili.

Dujaili ameongea kuhusu historia ya Imamu Ali Alhadi (a.s) na namna alivyo pambana na waovu wa zama zake, hadi akapewa sumu kama walivyo pewa babu zake watakasifu (a.s).

Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma tenzi na kaswida za kuomboleza zilizo amsha hisia ya huzuni na majonzi katika nyoyo za waumini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: