Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya warsha ya kuwajengea uwezo watumishi wapya wa chuo kikuu cha Al-Ameed.
Warsha hiyo ni sehemu ya ratiba ya kuongeza uwezo wa watumishi wapya na kuwafanya waendane na ubora unaotakiwa.
Warsha hiyo inafanywa ndani ya majengo ya shule za Al-Ameed kitengo cha (wasichana), mihadhara mbalimbali imetolewa kwa lengo la kuelekeza watumishi waliojiunga na chuo hivi karibuni.
Ratiba hiyo itadumu kwa muda wa wiki mbili.