Kamati ya majaji wa shindano la zawadi ya vizito viwili imepongeza Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu

Kamati ya majaji wa shindano la zawadi ya vizito viwili imepongeza hati ya msahafu mtukufu uliochapishwa na Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya.

Pongezi hizo zimetolewa baada ya kamati inayojumuisha wataalamu wa hati za Misahafu na kiarabu, ambao ni: Ustadh Auni Naqaashi na Ustadh Sayyid Nabiil Quraishi, kutembelea ofisi za Majmaa-Ilimi ya Qur’ani tukufu.

Kamati imekutana na rais wa Majmaa-Ilmi Dokta Mushtaqu Ali, msaidizi wake Ustadh Balasim Shimri, Meja Jenerali Abdulhussein na mkuu wa kituo cha uchapishaji wa misahafu Shekhe Dhiyaau-Dini Zubaidi.

Ziara hiyo ni sehemu ya ufuatiliaji wa kazi za washiriki wa shindano, ili waweze kupanga matokeo na kumpata mshindi wa kwanza wa shindano la (Zawadi ya vizito viwili) la hati za msahafu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: