Kituo cha utamaduni wa familia kimehitimisha program ya mlezi bora

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abasiyya tukufu, kimehitimisha program ya (mlezi bora) kwa familia za watu wenye mazingira magumu.

Kiongozi wa kituo bibi Sara Alhafaar amesema “Program hii inalenga wanawake wanaotoka kwenye familia za watu wenye mazingira magumu, wamefundishwa siku moja kwa wiki, wamekuwa wakipewa mihadhara ya saikolojia, dini, maadili na afya, sambamba na masomo ya ujasiriamali na ushojani”.

Akaongeza kuwa “Program inalenga kuwajengea uwezo wasichana wanaotoka kwenye mazingira magumu, na kuwasaidia waweze kuishi Maisha mazuri chini ya mwenendo wa Ahlulbait (a.s)”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Alhafaar “Kituo kinajipanga kufanya program nyingine, itakayo husisha tabaka zote za wasichana, kwa lengo la kuweka utulivu katika familia za wairaq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: