Chuo kikuu cha Al-Ameed kimesema: Tuliandaa kila anachohitaji mwanafunzi katika kufanya mtihani

Chuo kikuu cha Al-Ameed kimesema kuwa, tuliandaa kila anachohitaji mwanafunzi kwenye chumba cha mtihani kwa ajili ya mitihani ya nusu mwaka.

Makamo mkuu wa taaluma Dokta Maitham Hamidi Qambari amesema “Chuo kikuu cha Al-Ameed kilianza maandalizi ya mitihani kwenye kitivo cha famasia na uuguzi wiki kadhaa zilizopita, kimeweka mazingira mazuri ya ufanyaji wa mitihani”.

Akaongeza kuwa “Chuo kiliandaa kumbi maalum za kufanyia mitihani na kuweka vifaa vyote vinavyohitajika wakati wa mitihani, sambamba na kuteua wasimamizi wa mitihani”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Qambari, mitihani ya chuo ilianza tarehe (18/01/2023m) kwa kufuata ratiba iliyotolewa na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: