Majmaa-Ilmi imefanya hafla ya mimbari za nuru katika mkoa wa Kirkuuk

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya (mimbari za nuru) katika mtaa wa Taazah mkoani Kirkuuk.

Hafla imesimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa, kwa kushirikiana na kikundi cha vijana wa Zaharaa (a.s).

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Sayyid Muhammad Ridhwa Zubaidi, na kisomo maridhawa cha mahadhi ya kiiraq kutoka kwa Haidari Albazuni na msomaji wa Daarul-Qur’ani katika mji wa Taazah Sayyid Mussawi Abbasi Zamaan, sambamba na visomo tofauti kutoka kwa wasomaji wa kituo.

Hafla imefanywa ndani ya ukumbi wa Husseiniyya ya Imamu Mahadi (a.f) na kuhudhuriwa na watu wengi wapenzi wa kitabu cha Mwenyezi Mungu Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: