Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika kuadhimisha Ahlulbait (a.s) waliozaliwa ndani ya mwezi wa Rajabu.
Hafla hiyo imesimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa, kupitia mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa.
Rais wa Majmaa Dokta Mushtaqu Ali amesema: “Mradi wa kiongozi wa wasomaji, umeadhimisha kumbukumbu ya Ahlulbait (a.s) waliozaliwa katika mwezi wa Rajabu”.
Akaongeza kuwa “Katika hafla hiyo ameshiriki msomaji bwana Ibrahim Abdullahi na Hussein Alhajaar miongoni mwa wanafunzi wa mradi, na muimbaji wa qaswida za husseiniyya bwana Hassan Alkatrani”.
Mkuu wa mradi Sayyid Muhammad Ridhwa Azubaidi amesema: “Hafla hiyo wameshiriki wanafunzi wa mradi”, akabainisha kuwa “Mradi unahusisha masomo ya hukumu za usomaji wa Qur’ani na mihadhara mbalimbali ya kidini”.