Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umewasiri katika mji mkuu wa Sirya Damaskas, kwa ajili ya kuratibu harakati kwenye malalo ya Bibi Zainabu (a.s) kufuatia maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa baba yake (a.s).
Ugeni wa Ataba tukufu unaongozwa na mjumbe wa kamati kuu Sayyid Jawaad Hasanawi, umekutana na muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu nchini Sirya Mheshimiwa Shekhe Abdulhaliim Bahbahani.
Hasanawi amesema “Kukutana na muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu ni sehemu ya utaratibu wa Atabatu Abbasiyya ndani na nje ya Iraq, tumewasilisha salamu za kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya na katibu mkuu, sambamba na kumuonyesha ratiba itakayo tekelezwa katika malalo ya Bibi Zainabu (a.s)”.
Mwisho wa kikao hicho Mheshimiwa Shekhe Abdulhaliim akapongeza kazi kubwa inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s), likiwemo tukio hili tukufu.
Tambua kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imetuma ugeni maalum katika malalo ya Bibi Zainabu (a.s) nchini Sirya, kwa ajili ya kufanya harakati tofauti za kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Ali (a.s), pamoja na kuomboleza kifo cha jabali wa Subira (a.s).