Idara ya maelekezo ya kidini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya inafanya shindano la kimtandao liitwalo (Ghauthul-Waraa) katika kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Ali (a.s) mwezi kumi na tatu Rajabu.
Kiongozi wa idara Bibi Adhraa Shami amesema “Kufuatia kukaribia siku aliyozaliwa kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s), idara yetu imeamua kuendesha shindano hili kwa lengo la kuimarisha elimu ya Dini katika jamii”.
Akaongeza kuwa “Wasichana kutoka mikoa yote hapa nchini wanakaribishwa kushiriki, tumeandaa zawadi za washindi watatu wa mwanzo, tambua kuwa iwapo kutakuwa na washindi watakao gongana katika nafasi tatu za mwanzo tutapiga kura ya kuwapata washindi watatu siku ya kuadhimisha mazazi hayo matukufu”.
Kwa mujibu wa Shami: “Fomu ya ushiriki wa shindano kwa njia ya mtandao itatolewa siku ya mwezi 9 Rajabu, na watu wataendelea kujibu maswali kupitia fomu hiyo hadi mwezi 13 Rajabu siku aliyozaliwa Imamu Ali (a.s)”.