Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kimetaja siku ya uzinduzi wa Sardabu ya Imamu Hussein (a.s), iliyopo ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kitengo kimesema kuwa siku ya ufunguzi wa Sardabu itakuwa ni siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini (a.s) ambayo ni mwezi kumi na tatu Rajabu.
Sardabu hiyo inasehemu maalum ya wanawake na sehemu ya watoa huduma, imejengwa chini ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na itaingiza idadi kubwa ya mazuwaru, hivyo itapunguza msongamano wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.