Mazingira ya furaha yametanda katika Atabatu Abbasiyya kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kiongozi wa waumini (a.s).

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, umefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s).

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Sayyid Aqiil Yaasiri amesema “Hafla hiyo imeandaliwa kwa kushirikiana na kitengo kinacho simamia haram tukufu kwa lengo la kuadhimisha kumbukumbu za watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Rajabu”.

Akaongeza kuwa “Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na ujumbe kutoka kitengo cha Dini ulio eleza utukufu wa kiongozi wa waumini na historia yake (a.s)”.

Hafla imepambwa na mashairi ya Umudi na Shaabi kutoka kwa kundi la washairi, beti za mashairi yao zimetaja historia ya Mtume na utukufu wa watu wa nyumbani kwake (a.s), mbele ya kundi kubwa la mazuwaru na wahudumu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa mujibu wa maelezo ya Yaasiri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: