Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wametandika miswala mipya ndani ya haram tukufu.
Utandikaji wa miswala mipya umefanywa sambamba na maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s).
Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Zainul-Aabidina Adnani Quraishi amesema “Wahudumu wa kitengo cha kusimamia haram tukufu wametandika miswala (mazulia) mapya ndani ya haram tukufu”, akaongeza kuwa “Mazulia yaliyo tandikwa ni maalum na yanaendana na mapambo yaliyopo haram ikiwa ni pamoja na kashi Karbalai”.
Kazi ya kutandika mazulia imefanywa kwa kushirikiana na idara ya masayyid wanaotoa huduma katika Ataba tukufu, kitengo cha kulinda nidhamu na kitengo cha utumishi, kwa mujibu wa maelezo ya Kuraishi.