Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia mradi wa (Dhibiti kipaji) kimewapongeza wanafunzi walioshiriki kwenye visomo vya kiarabu.
Kiongozi wa mradi huo bwana Amru Alaa Alkifaai amesema “Kitengo kimepokea kundi la wanafunzi, waliowakilisha Iraq kwenye shindano la kimataifa la visomo vya kiarabu, na wakapata ushindi kwenye shindano hilo”.
Akaongeza kuwa “Kitengo kimewaandalia ratiba maalum ya kuwapongeza iliyodumu kwa muda wa siku mbili, inahusisha kutembelea vituo vya kitamaduni na mji wa Sayyid Auswiyaa, na sehemu zingine za mji wa Karbala na wakahitimisha kwa kukutana na rais wa kitengo”.
Akasisitiza kuwa “Mradi umejikita katika kuendeleza vipaji vya vijana, na kuwasaidia katika ubunifu wao ili waweze kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa”.