Atabatu Abbasiyya imeshiriki kwenye shughuli za maombolezo katika malalo ya Bibi Zainabu (a.s) kwenye kumbukizi ya kifo chake na imepandisha bendera zinazo ashiria huzuni na majonzi.
Rais wa kitengo cha usimamizi wa haram Sayyid Khaliil Hanuun amesema “Ataba tukufu za Iraq zimekua zikishiriki kwenye maombolezo ya kifo cha Bibi Zainabu (a.s) katika haram yake takatifu jijini Damaskas nchini Sirya kwa miaka mingi”.
Akaongeza kuwa: “Kuna shughuli tofauti ambazo hufanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu wakati wa maombolezo, ikiwa ni pamoja na kuweka mapambo meusi katika haram ya Bibi Zainabu (a.s)”.
Idara ya ushonaji katika kitengo cha zawadi na nadhiri huandaa vitambaa na kuvidarizi baadhi ya jumbe zinazo ashiria huzuni.
Shughuli za uombolezaji katika malalo ya Bibi Zainabu (a.s) husimamiwa na Atabatu Abbasiyya chini ya mjumbe wa kamati kuu Sayyid Jawadi Hasanawi na baadhi ya wajumbe wengine wa kamati kuu pamoja na marais wa vitengo.