Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, inafanya warsha ya kuwajengea uwezo walimu wake yenye anuani isemayo (Mbinu za utambuzi wa maumbile).
Kiongozi wa Maahadi Bibi Manaar Aljaburi amesema “Warsha hii ni sehemu ya mradi wa kujenga uwezo wa walimu, mkufunzi ni Ustadh Murtadha Zaki Tamimi, mbobezi wa elimu ya nafsi kutoka kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Ataba tukufu”.
Akasisitiza kuwa “Maahadi inatilia umuhimu mkubwa katika kufanya semina na warsha za kujenga uwezo wa walimu wake na kuwafanya waendane na maendeleo ya sasa”.