Wahudumu wa Ataba mbili wanaomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s)

Wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kupitia maukibu ya pamoja, wameomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s).

Wamefanya matembezi ya amani kuanzia kwenye haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakapitia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, wakati wa matembezi hayo wameimba kaswida za kuomboleza zilizo amsha hisia za huzuni na majonzi katika nyoyo za wapenzi wa Ahlulbait (a.s).

Maikibu ilipowasili katika haram ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s), imefanya majlisi ya kuomboleza iliyohudhuriwa na kundi kubwa la mazuwaru, hapo zikaimbwa kaswida na tenzi za kuomboleza zilizo eleza mambo yaliyotokea katika vita ya Twafu, na jinsi alivyo simama imara kumnusuru kaka yake Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: