Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya uliopo Sirya umefanya majlisi ya kuomboleza ndani ya malalo ya Bibi Zainabu (a.s) katika kumbukizi ya kifo chake.
Makamu katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Murtadha Hussein Zaini amesema “Harakati za Atabatu Abbasiyya tukufu nchini Sirya, zinahusisha kufanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Majlisi itadumu kwa muda wa siku tatu baada ya swala ya Adhuhuri na Alasiri, hufanywa kwa kushirikiana na Atabatu Zainabiyya”.
Akabainisha kuwa “Majlisi za kuomboleza zinaeleza historia ya Bibi Zainabu (a.s) na kazi kubwa aliyofanya katika kumnusuru kaka yake Imamu Hussein (a.s) na namna alivyo fanikiwa kufikisha ujumbe kwa wafuasi wote wa Ahlulbait (a.s)”.
Majlisi hizo zinapata mahudhurio makubwa ya waombolezaji, sambamba na utoaji wa huduma ya chakula kwa mazuwaru wa Bibi Zainabu (a.s).