Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya hafla za (mimbari za nuru) katika kumbukumbu ya kifo cha Bibi Zainabu (a.s).
Hafla hizo zinasimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na wasomaji mbalimbali wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, miongoni mwa wasomaji walioshiriki ni: Hussein Hamuud, Hussein Ali na msomaji wa Ataba mbili bwana Osama Karbalai.
Hafla iliyofanywa ndani ya msikiti wa Majmaa-Alqami, imepata mahudhurio makubwa ya watumishi na wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa.
Hafla ikahitimishwa kwa Qaswida na tenzi zilizosomwa na Mulla Abbasi Twalibawi, zikakumbusha kifo cha Bibi Zainabu (a.s).