Ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani imetoa tamko kuhusu tetemeko lililotokea Uturuki na Sirya.
Ifuatayo ni nakala ya tamko kama lilivyo andikwa kwenye ukurasa maalum wa ofisi ya Marjaa Dini mkuu.
“Hakika tetemeko lililotokea hivi karibuni katika nchi ya Uturuki na Sirya (kwa mujibu wa vyombo vya habari) limesababisha vifo vya watu wengi na hasara kubwa ya mali, hili ni janga la kibinaadamu ambalo halijashuhudiwa janga kama hilo katika zama hizi.
Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu anatoa salamu za rambirambi kwa ndugu na jamaa walio poteza wapendwa wao, na anaungana na wahanga wote wa janga hilo, anamuomba Mwenyezi Mungu awape subira na kuwaponya haraka majeruhi wote, aidha anaomba vikundi vya uokozi na wahisani mbalimbali wajitokeze kwa wingi kutoa msaada wa haraka kwa waathirika wa janga hilo.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atuondolee balaa na atupe neema ya amani na utulivu, hakika yeye ni muweza wa hilo na mwingi wa kurehemu”.