Kitengo cha maarifa ya kiislamu kinafanya nadwa kuhusu familia za kusini mwa Iraq

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimefanya nadwa yenye anuani isemayo (Familia za visiwani kati ya jografia ya sehemu na utamaduni wa koo).

Nadwa imesimamiwa na kituo cha turathi za kusini chini ya kitengo.

Mtoa mada katika nadwa hiyo alikua ni Dokta Ahmadi Fadhili Ajimi, ameeleza kwa urefu visiwa vya kusini mwa Iraq na mipaka yake kijografia kuanzia Huur Himaar adi Huur Hawizah na sababu za kuitwa hivyo, akataja koo za visiwani zilizo ishi maeneo hayo.

Nadwa imejikita katika kueleza taasisi za turathi za kusini na namna ya kuzitunza, aidha washiriki wametoa ushirikiano mzuri, wameuliza maswali na kutoa maoni mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: