Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi ametembelea mradi wa malezi na elimu unaotekelezwa na kitengo cha malezi na elimu ya juu katika muhula wa pili wa masomo.
Kuna mpango mkakati maalum wa muhula wa pili wa masomo katika mwaka huu 2023 unaoendana na misingi ya malezi, elimu, uzalendo na Dini.
Rais wa kitengo hicho Dokta Hassan Daakhil Karim amemuambia kiongozi mkuu wa kisheria kuwa, tumekamilisha selebasi ya muhula wa kwanza wa masomo, sasa hivi tunajiandaa na muhula wa pili, akaeleza miradi ya malezi ya baadae itakayofanywa na shule za Al-Ameed.
Kiongozi mkuu wa kisheria amehimiza umuhimu wa kusaidia watumishi na kuwawezesha kutekeleza wajibu wao kwa weledi na uaminifu mkubwa.