Kituo cha utamaduni wa familia kinaratibu mihadhara elekezi

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya, kinaratibu mihadhara elekezi kwa anuani isemayo (Njia za kudhibiti hasira).

Kiongozi wa kituo bibi Sara Alhafaar amesema “Mihadhara inalenga kundi la wasichana, imetolewa kupitia mitandao ya kijamii iliyochini ya kituo”.

Akaongeza kuwa “Mhadhara uliotolewa na Sundusi Muhammad, umeangazia matukio ambayo husababisha hasira na namna ya kuzuwia hasira”.

Kwa mujibu wa Alhafaar “Mihadhara elekezi itaendelea kutolewa mara mbili kila mwezi, kwa lengo la kuongoza nafsi na familia, sambamba na kumfundisha mwanamke mbinu za kuongoza familia, kwa lenga la kuzifanya kuwa na utulivu na amani chini ya mwenendo wa Ahlulbait (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: