Majmaa-Ilmi inaendelea na harakati za Tablighi kwa mazuwaru wa Imamu Alkaadhim (a.s)

Majmaa-Ilmi katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea na harakati za Tablighi kwa mazuwaru wa malalo ya Imamu Alkaadhim (a.s) wanaokwenda kuomboleza msiba wake.

Kiongozi wa idara ya Tablighi Sayyid Ahmadi Zaamiliy amesema “Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa-Ilmi imeweka vituo vitano vya Tablighi kaskazini ya mkoa wa Waasit uliopo zaidi ya kilometa (20), kila kituo kinamhadhiri, mtu wa kujibu maswali ya kisheria, watu watatu wanaosahihisha usomaji wa surat Faat-ha na baadhi ya sura fupi zinazo somwa mara nyingi kwenye swala na nyeradi za swala”.

Akaongeza kuwa “Maahadi imetuma ugeni wenye mubalighina watano, wasomaji wa Qur’ani kumi na tatu pamoja na watu waliofadhi Qur’ani tukufu, katika mkoa wa Waasit kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru wanaotembea kwa miguu kwenda Bagdad kushiriki uombolezaji wa kifo cha Imamu Mussa Alkaadhim (a.s) kwa kutoa maelekezo ya kidini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: