Ugeni kutoka Baabil wamepongeza mfumo wa ufundishaji unaotumiwa na kitengo cha malezi na elimu ya juu

Ugeni kutoka mkoa wa Baabil, umepongeza mfumo wa kisasa unaotumiwa na kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Muwakilishi wa kitengo Dokta Aadil Kuraishi amesema “Watu wengi huja kuangalia miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, sambamba na mfumo wa kisasa unaotumiwa na kitengo cha malezi na elimu ya juu katika ufundishaji”.

Hakika kitengo kinafanya kila kiwezalo kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwenye sekta ya elimu sambamba na maendeleo ya taifa katika mambo mengine.

Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Shekhe Aamir Ma’amuuri amesema kuwa “Ugeni umetembelea shule za Al-Ameed na kuangalia sehemu muhimu za shule”.

Ugeni umepongeza mfumo wa ufundishaji unaotumiwa na kwamba utaleta mafanikio makubwa kwenye sekta ya elimu hapa nchini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: