Atabatu Abbasiyya inafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Alkadhim (a.s)

Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Mussa Bun Jafari Alkadhim (a.s).

Majlisi imefanywa kwa kushirikiana kati ya kitengo cha mahusiano na idara ya Tablighi ndani ya ukumbi wa utawala, imehudhuriwa na idadi kubwa ya watumishi na mazuwaru.

Majlisi hiyo ni sehemu ya ratiba ya uombolezaji katika Atabatu Abbasiyya, itakayo dumu kwa muda wa siku mbili, imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu.

Siku ya kwanza ameongea Shekhe Haani Shabani, ameeleza historia ya Imamu Alkadhim (a.s) na msimamo wake sambamba na kueleza ubora wa tabia zake na uaminifu wake.

Majlisi ikahitimishwa kwa usomaji wa tenzi kuhusu Imamu Mussa Alkadhim (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: