Watumishi wa Ataba mbili wanaomboleza kifo cha Imamu Alkaadhim (a.s)

Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, wanaomboleza kifo cha Imamu Alkaadhim (a.s) kupitia maukibu ya pamoja.

Maukibu imeanzia katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ikapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu ikaenda hadi kwenye haram ya Imamu Hussein (a.s).

Wakati wa matembezi hayo walikuwa wanaimba kaswida za huzuni zilizo amsha hisia za majonzi katika nyoyo za waumini na wapenzi wa Ahlulbait (a.s).

Baada ya kuwasili katika haram ya Imamu Hussein (a.s), wakafanya majlisi ya kuomboleza ambayo mazuwaru wameshiriki, tenzi na kaswida mbalimbali zilizo eleza dhulma alizofanyiwa Imamu Alkaadhim (a.s), zimesomwa kwenye majlisi hiyo, msimamo wa Imamu (a.s) ulikuwa ni kumfanyia wema anayemfanyia mabaya na kuzuwia hasira.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: