Ugeni kutoka kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, umejadili njia za kushirikiana na taasisi za wanawake katika nchi ya Seralion.
Mkuu wa Markazi Dirasaat Afriqiyya Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema kuwa “Ugeni umekutana na wakuu wa taasisi ya bibi Zaharaa (a.s) katika nchi ya Seralion, na kujadili namna ya kushirikiana na taasisi za wanawake katika Atabatu Abbasiyya kwa lengo la kufanya miradi ya kidini na kitamaduni”.
Akaongeza kuwa “Muwakilishi wa Idara ya Tablighi katika Markazi Sayyid Muslim Aljaabiri, amefanya mazungumzo na kiongozi wa taasisi ya Zaharaa (a.s), akaeleza shughuli zinazofanywa na Markazi Dirasaat Afriqiyya na harakati za kidini na kitamaduni katika bara la Afrika”.
Shimri akabainisha kuwa “Taasisi ya bibi Zaharaa (a.s) hufanya harakati za kimasomo, kibinaadamu na kiuchumi”.