Kamati ya elimu na maandalizi ya kongamano la (wiki ya Uimamu) litakalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya kwa mara ya kwanza, zimejadili hatua ya mwisho ya maandalizi ya kongamano hilo.
Wiki ya uimamu ni kongamano la kitamaduni na kimataifa litakalo fanywa kwa muda wa siku saba mfululizo, litasimamiwa na Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na Jumuiya ya Al-Ameed, chuo kikuu cha Alkafeel na chuo kikuu cha Al-Ameed.
Katika kikao hicho imependekezwa kuunda kamati ya elimu yenye wajumbe kutoka pande zote zinazoshiriki kuandaa kongamano hilo, itakayo simamia upokeaji wa mada zitakazo wasilishwa kwenye kongamano, sambamba na kuunda kamati maalum ya habari.
Aidha kikao hicho kimefanya baadhi ya marekebisho, kumbuka kongamano litakuwa na harakati mbalimbali za kitamaduni.