Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimekamilisha ratiba ya kitamaduni kwa vijana wa mkoa wa Diwaniyya.
Ratiba hiyo imesimamiwa na kituo cha Multaqal-Qamaru chini ya kitengo.
Mkuu wa kituo Shekhe Haarith Daaji amesema “Kituo kimekamilisha ratiba ya kitamaduni iliyoandaliwa kwa ajili ya vijana wa mkoa wa Diwaniyya, chini ya mkakati wa kujenga vijana kielimu na kimaadili”.
Akaongeza kuwa “Wageni wamekuwa wakipokelewa kwa muda wa siku mbili, kituo kimewasilisha mihadhara inayohusu Dini, utamaduni na maendeleo ya kibinaadamu, sambamba na kujadili changamoto wanazokumbana nazo vijana na kuonyesha utatuzi wa changamoto hizo unaofaa”.
Ratiba hiyo imepambwa na matembezi ya kuangalia miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ikiwa ni pamoja na kutembelea shamba la mikunazi na kufanya majlisi huko, sambamba na majlisi za kimalezi na kitamaduni zinazo msaidia mshiriki kuwa mfano katika jamii, kwa mujibu wa maelezo ya Daahi.